HomeRadio Vaticana
foto testata  

Categories


  Charity & Solidarity


  Church


  Culture & Society


  Vatican Documents


  Synod


  Ecumenism


  Family


  Youth


  Justice & Peace


  Politics


  Religion & Dialogue


  Science & Ethics


  Audiences
   & Angelus



  Pastoral visits


cx_t09

CTV - You tube

CTV



 home > Ecumenism > news


06/11/2009 14.55.25



Askofu mteule Festo Ngowo wa KKKT dayosisi ya Dodoma kusimikwa rasmi jumapili ijayo!






Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania, KKKT., Dayosisi ya Dodoma Mhashamu Festo Ngowo anatarajiwa kusimikwa rasmi siku ya jumapili tarehe 8 Novemba, 2009 kushika nafasi ya Askofu Peter Mwamasika aliyestaafu shughuli za kichungaji baada ya kuitumia Dayosisi ya Dodoma kwa kipindi cha miaka ishirini na moja.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kaimu katibu mkuu wa kanisa la KKKT Dayosisi ya Dodoma, mchungaji Victoria Ntega anasema kwamba, ibada kwa ajili ya kusimikwa askofu mteule Festo Ngowo itaanza majira ya saa 3 asubuhi kwenye kanisa kuu la KKKT, mjini Dodoma na itaongozwa na mkuu wa kanisa hilo Askofu mkuu Alex Malasusa.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ibada hiyo itahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini na serikali akiwemo Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Askofu Yuda Thadei Ruwaich.
Aidha wageni wengine walioalikwa wametoka katika nchi za Marekani, Ujerumani, Sweeden na Maaskofu kutoka katika makanisa ya mkoa wa Dodoma na mikoa ya jirani.
Katika Ibada hiyo ya kumsimika askofu Ngowo pia kutakuwepo na tukio la kutunukiwa shahada ya heshima kwa mkuu wa kanisa hilo Askofu mkuu Alex Malasusa.


  « back to index

 






09/11/2009 13.51.16
Askofu Festo Ngowo asimikwa rasmi kuliongoza Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Dayosisi ya Dodoma


09/11/2009 10.15.06
Mikakati ya kudhibiti madhara ya tabianchi ni dhamana ya kimaadili kwa viongozi wa kimataifa


23/10/2009 12.02.22
Ecumencal progress in London and Rome.


24/09/2009 11.06.37
Mwanadamu anahesabiwa haki mbele ya Mungu kwa njia ya maisha, kifo na ufufuko wa Kristo!


22/09/2009 9.32.57
Dunia inakabiliwa na mtikisiko wa kiuchumi na mmong'onyoko wa kimaadili



Related categories


Page précédente  Previous page
Page d'accueil  Home Page
Ecrire à la rédaction  Contact us
top
top
All the contents on this site are copyrighted ©. Webmaster / Credits / Legal Conditions
top
top