HomeRadio Vaticana
foto testata  

Categories


  Charity & Solidarity


  Church


  Culture & Society


  Vatican Documents


  Synod


  Ecumenism


  Family


  Youth


  Justice & Peace


  Politics


  Religion & Dialogue


  Science & Ethics


  Audiences
   & Angelus



  Pastoral visits


cx_t07

CTV - You tube

CTV



 home > Culture & Society  > news


07/11/2009 10.38.06



Benedikto XVI asema: michezo ina nafasi ya pekee katika maisha na majiundo ya vijana kiroho na kimwili






Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita katika ujumbe wake aliomwandikia Kardinali Stanslaw Rylko, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya walei pamoja na washiriki wote wa semina inayojadili kuhusu michezo, elimu na imani katika mwelekeo mpya wa shughuli za michezo anasema, michezo ina nafasi ya pekee katika maisha ya vijana, majiundo ya mtu mzima na matumizi sahihi ya muda.

Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican anasema Baba Mtakatifu unatambua dhamana na nafasi ya michezo katika majiundo ya mtu kimaadili, kiutu na kikristo katika ulimwengu wa kizazi kipya. Ni fursa ya kuboresha mwili wa mtu na shule makini ya tunu msingi za kiutu, kibinadamu na katika maisha ya kiroho. Michezo ikitumiwa vyema kama sehemu ya majiundo ya mtu mzima inakuwa ni fursa kwa viongozi wa Kanisa kuwasaidia vijana katika majiundo yao.

Baba Mtakatifu anasema, Kanisa litaendelea kuwekeza katika michezo kwa vijana, likiwasaidia kujenga tunu bora zinazoibuliwa katika michezo kama vile ushindani, ujasiri na ari ya kufikia malengo yaliyowekwa; hali wakijitahidi kukwepa mambo yote yanayoweza kuharibu nafasi ya michezo katika maisha ya vijana.

Vijana wanapaswa kutumia vyema nafasi ya michezo, ili kuendeleza vipaji na karama zao, sanjari na tunu za kiutu na kikristo ili kufikia ukomavu kamili. Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita analipongeza Baraza la Kipapa kwa ajili ya walei kwa kuandaa semina kama hii, ili kutoa mwelekeo wa Kanisa katika masuala ya kichezo. Michezo ni fursa nzuri ya shughuli za kitume kwa vijana.


  « back to index

 






10/11/2009 14.01.32
UNESCO kutoa tuzo kwa wadau katika kudumisha amani na uvumilivu ndani ya jamii


09/11/2009 10.55.27
Shirikisho la Umoja wa Radio Barani Afrika linajiandaa kwa Mashindano ya Kombe la Dunia 2010


06/11/2009 13.07.04
Mount Kilimanjaro's glaciers have lost 85% of the ice they had in 1912.


06/11/2009 11.15.30
Askofu mkuu Ravasi asema: Kanisa linapenda kukuza urafiki na majadiliano na wasanii


24/10/2009 13.07.03
Stop destroying the planet as if there was no tomorrow. A plea by Pope Benedict and the Ecumenical Patriarch Bartholomew lst.



Related categories


Page précédente  Previous page
Page d'accueil  Home Page
Ecrire à la rédaction  Contact us
top
top
All the contents on this site are copyrighted ©. Webmaster / Credits / Legal Conditions
top
top