07/11/2009 11.47.03


"Jamii ya watanzania si takatifu wala kamilifu inaelemewa na dhambi ya kutotimiza wajibu"


|

Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Tanzania hivi karibuni amesema, Tanzania inatarajia kutumia kiasi cha shilingi Billioni mia moja na sita, ili kufanikisha uchaguzi mkuu 2010.
Baadhi ya nchi wafadhili wanakusudia kuchangia kiasi hicho cha fedha ili kufanikisha zoezi la uchaguzi mkuu. Maboresho ya daftari la wapiga kura, ununuzi wa vifaa vya uchaguzi, elimu ya uraia, ugawaji wa majimbo na ufumbuzi wa migogoro ya uchaguzi ni kati ya changamoto zinazoikabli Tume ya Uchaguzi Tanzania.
Askofu mkuu Paul Ruzoka, Mwenyekiti wa Tume ya Haki na Amani, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, katika mahojiano maalum na Radio Vatican anafafanua kwa kina juu ya Barua ya kichungaji iliyotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, inayoongozwa na mada "Enyi watu wangu sikieni sheria yangu" Kanisa Katoliki Tanzania linatambua kwamba, jamii ya watanzania si takatifu wala kamilifu, kwani bado inaelemewa na dhambi ya kutotimiza wajibu.
Dhamiri safi anasema Askofu Ruzoka ni dira ya Tanzania. Waraka wa Maaskofu ni wajibu wa kiraia na kwamba Ilani ya Uchaguzi inayopembua vipaumbele kwa Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu hapo 2010. Ninakukaribisha uweze kumsikiliza kwa majini Askofu Mkuu Ruzoka akifafanua kuhusu Waraka wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.
|